Kila siku kwa miaka miwili, afisa wa
Korea Kusini amechukua simu yenye rangi ya kijani na kumpigia afisa
mwenzake upande wa pili , nje tu ya mpaka wa Korea Kaskazini. Lakini
hamna aliyejibu simu hiyo.
Hayo yote yakabadilika saa 9.30 ( 6.30
saa za GMT) tarehe 3 Januari 2018. Katika muda wa dakika 20,pande zote
mbili walitumia laini zao wakiwa na matumaini ya kupungunza ugomvi baina
ya nchi zao za Korea.Simu hiyo ipo katika kijiji cha mpaka wa Panmunjom, ambapo pamekuwa chanzo cha mawasiliano baina ya majirani hao ambao kimsingi bado wako vitani. Lakini tunafahamu nini kuhusu simu hiyo?
'Hamna Utani'
Ni jambo linalokaa kama limetoka moja kwa moja katika nyakati za vita vya baridi - ni kweli. Likijengwa kwenye dawati mbalo ziliwekwa simu zenye rangi ya kijani na nyekunde pamoja na kompyuta, laini ya Kusini na Kaskazani ilizinduliwa mwaka 1971 kwa minajili ya mawasiliano kati ya shiriki la msalaba mwekundu wa Korea Kaskazani na Korea Kusini.Laini za ziada zilizinduliwa mwaka 1972 wakati wa maongezi kuhusu kuunganishwa kwa nchi hizo mbili tena mwaka 1990 na 2000
Hii leo kuna takribani laini 33 kati ya korea hizi mbili, tano kati yake ni kwa ajili ya mawasiliano ya kila siku, 21 ni kwa ajili ya mazungumzo baina yao korea, 2 ni kwa ajili ya maswala ya anga, mbili kwa ajili ya maswala usafiri majini na tatu kwa ajili ya mashirikiano ya kuichumi na kibiashara
Lakini zimekuwa hazifanyi kazi tangu mwezi wa pili 2016 wakati Korea ya kaskazini ilipovunja mahusiano na kusini baada ya Seoul kusitisha mradi wa ushirika wa kiuchumi wa Kaesong Industrial Complex baada ya Pyongyang kufanya jaribio ya lanyuklia
0 Comments In "Je unazifahamu simu 'nyekundu na kijani' zilizotumika na nchi za Korea Kusini na Kaskazini?"